Faida za kuingia katika Uislamu

Kuingia katika Uislamu kuna faida nyingi kwa mtu mmoja na jamii kwa kuwa Uislamu unategemea dalili na ushahidi, tutataja dalili za Kiungu kwa kila faida kwa maana ambayo hakuna mtu anayeweza kudhamini faida hizo isipokuwa Muumba wetu Mtukufu Aliyetukuka.

1-Mlango wa pepo ya milele.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: { Na wabashirie walio amini na wakatenda mema kwamba watapata mabustani yapitayo mito kati yake…}Surat Al-Baqara aya ya ( 25) Ikiwa utaingia peponi utaishi humo maisha ya furaha, hakuna maradhi, maumivu,huzuni, au kifo na Mwenyezi Mungu atakuridhia na utaishi humo milele na milele.

2-Furaha ya kweli na usalama wa ndani.

Furaha ya kweli na usalama wa ndani hautapatika isipokuwa kwa kutii amri za Muumba mwenye kuruzuku ulimwengu huu.
Muumba wetu Mtukufu Aliyetukuka anasema: {Hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutulia}Surat Ar-Rad aya ya (28) Kwa upande mwingine, mtu aliyejitenga na Qur'an atakuwa na maisha ya shida katika ulimwengu huu, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki..}Surat Twaha aya ya (124)

3-Kuokoka kutokana na moto.

Muumba wetu Mtukufu anasema:{Hakika wale walio kufuru,na wakafa hali ni makafirihaitakubaliwa kutoka kwa yeyote wao fidia ya dhahabu ya kujaza dunia nzima lau wangeli itoa. Hao watapata adhabu chungu, wala hawatakuwa na wa kuwanusuru} Surat Al-Imran aya ya (91)

Kwa hiyo, maisha katika ulimwengu huu ni nafasi pekee ya sisi kushinda peponi na kuoka kutokana na moto kwa sababu kama mtu akifa kwa kutoamini hana nafasi nyingine ya kurudi duniani ya kuwa mwamini.

4-Msamaha ni kwa dhambi zote zilizotangulia.

Watu wengi wana ona aibu na wao wana wasiwasi juu ya dhambi nyingi ambazo wamezifanya katika maisha yao yote, lakini kuingia katika Uislamu unafuta yaliyotangulia miongoni mwa madhambi kama vile hayakuwapo, kwa sababu Muislamu ni mpya ni safi kama mzaliwa mpya ambaye hana madhambi.
Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Waambie wale walio kufuru: wakikoma watasamehewa yaliyokwisha pita. Na wakiyarudia basi imekwisha pita mifano ya wa zamani} Surat Al-Anfaal aya ya (38)

5. Uhusiano wa moja kwa moja kwa Muumba wetu Mtukufu (mbali na muunganishaji yeyote):

Uislamu ni uhusiano wa moja kwa moja kati yetu na Muumba wetu Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa ajili ya kumuomba yeye Mtukufu na anatujibu maombi yetu. Muumba wetu Mtukufu anasema: {Na waja wangu watakapo kuuliza khabari zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anapo niomba. Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi,ili wapate kuoka}Surat Al-Baqara aya ya (186)

Tafadhali zungumza na sisi kwa maelezo zaidi na maswali juu ya Uislamu.


Chat